Afya ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe yaimarika, Hospitali ya KCMC Moshi, Kilimanjaro imesema hali ya Mbowe inaendelea vyema baada ya kuondolewa mashine ya oksijeni iliyokuwa inamsaidia kupumua.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha hivyo ambapo amesema kwa sasa anapumua mwenyewe bila msaada wa mashine hiyo.

Mbowe alifikishwa hospitalini hapo jana akiwa ameambatana na baadhi ya makada wa chama hicho, akiwa katika hali mbaya.

Hivyo katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema, Mbowe alianza kuugua gafla wakati akipata chakula cha mchana katika hoteli ya Keys, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

”Tulikuwa tukipata chakula cha mchana katika Hoteli ya keys mwenyekiti alisema anajisikia vibaya na afya yake haiko sawa hivyo akataka tumpeleke hospitali ya KCMC kwa ajili ya kuangalia afya yake” amesema Lema.

Hivyo alikimbizwa hospitali na madaktari wakashauri alazwe kwa matibabu na uchunguzi zaidi wa afya yake.

 

Mkwasa: Tunaitakia kila kheri Simba dhidi ya Al Masry
Video: DC Kasesela ajivunia kubadili fikra za wananchi Iringa