Klabu ya soka ya SImba kupitia kwa msemaji wake, Haji Manara imetoa utaratibu kwa mashabiki wake wanaotaka kusafiri na timu kwenda nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Al Masry.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Manara amesema kuwa tayari klabu imeshafanya utafiti wa gharama ambazo mashabiki wanatakiwa kulipa ikiwemo gharama za usafiri kiasi cha Dola 500 zaidi ya shilingi milioni moja ambazo zitatumika kwa ajili ya tiketi na Visa.
Amesema kuwa safari ya mashabiki inatarajiwa kufanyika ijumaa ya Machi 16 na watarejea Jumapili Machi 18 baada ya mechi kuchezwa Machi 17 siku ya Jumamosi.
Hata hivyo, Simba na Al Msry zinacheza leo mchezo wa kwanza Kombe la Shirikisho majira ya saa 12:00 jioni kwenye uwanja wa taifa na zitarudiana Machi 17 nchini Misri ili kupata mshindi wa jumla atakayefuzu hatua ya makundi.