Mwandishi wa habari ambaye amewahi kupata tuzo ya kuwa mwandishi bora wa mwaka 2010/2011, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Innovative media Solutions ltd, na shabiki nambari moja timu ya Young Africans, Yanga, aliyewahi kuwa msemaji wa timu hiyo, Jerry Muro ametoa funzo kubwa kwa watanzania namna ya kuwa wazalendo.
Jerry Muro kupitia kurasa wake wa instagram amerusha picha ikimuonesha yupo uwanja wa Taifa akishangilia timu ya Simba ambayo jana ilicheza na Timu ya Misri ya Al Masry na kufanikiwa kutoka kwa mabao sare 2-2, hali iliyompelekea shabiki huyo wa yanga kutoa pongezi za dhati kwa mtani wake Haji Manara kwa kazi nzuri ambayo vijana wake wameifanya uwanja wa Taifa.
Jerry Muro ameandika hivi kwenye ukurasa wake;
”Uzalendo ni Imani na Msingi wa Umoja na Mshikamano wetu, Mpira unatuleta pamoja Watanzania tusiruhusu Ushabiki uondoe uzalendo wetu katika Mambo Makubwa ya kimataifa, Hongera Swahiba sio haba @hajismanara #MzalendoHalisi #Umoja wetu.
-
Simba SC yajiweka njia panda kombe la shirikisho Afrika
-
Township Rollers yaibutua Young Africans Taifa
Huu ni uzalendo ambao watanzania wanapaswa kujifunza kwa Jerry, kwani siku za karibuni watu wameonekana kukosa uzalendo kwa kuleta utimu na kuuvua Utanzania wao na kusahau kuwa sisi sote ni wa moja sio mashabiki wa Simba sio mashabiki wa Yanga.
Hii ni kufuatia mechi zinazoendelea ambapo siku ya Juzi Yanga ilicheza na wageni wake toka Botswana, Rollers ambapo mchuano ulikua mkali na kufanikisha Rollers kuwafunga yanga goli 2-1, hali iliyoleta furaha kubwa sana kwa mashabiki wa Simba kuona watani wao wa jadi Yanga wameangukia pua kwenye mechi yao dhidi ya wageni wao.
Aidha michuano bado inaendelea tunaziombea timu zetu za jadi Yanga na Simba kufanya maandalizi ya mashambulizi ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika marudiano ya mechi zilizobakia zinazotarajiwa kufanyika nchini kwao.