Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania linatoa pole kwa Wauguzi kutokana na matukio yaliyofanywa na viongozi ikiwapo kuwekwa rumande na kupigwa katika mazingira yao ya kazi na limelaani vikali matukio hayo dhidi yao.

Taarifa hiyo imetolewa na Lena M. Mfalila na kusema kwamba vitendo hivyo ni udhalilishaji na ni kinyume cha miongozo ya kisheria inayosimamia ushughulikiaji wa tuhuma za uvunjifu wa nidhamu na sheria wakati wa kazi.

Taarifa hiyo ni kufuatia tukio lililotokea, tarehe 7/3/2018 katika Hospitali ya Wilaya ya Tandahimba ambapo Muuguzi Amina Luena Nicodemus aliwekwa ndani kwa amri ya Mkuu wa Wilaya kwa tuhuma za kuuza nguo za watoto akiwa kazini.

Pamoja na tukio lingine lililotokea tarehe 8/3/2018 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo Muuguzi Hilda Ebunka alipigwa na Diwani akiwa kazini akitoa huduma

Aidha Mfalila amesema kwamba kumpiga mtumishi wakati akiwa kazini ni udhalilishaji na ni kinyume cha sheria.

“Nidhamu ya Wauguzi na Wakunga inasimamiwa na sheria inayoitwa The Nursing and Midwifery Act, 2010 inayotoa mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu kwa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania”.  amnesema Mfalila.

Viongozi wa kitaifa, ikiwa ni pamoja na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Mheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa nyakati mbalimbali wamekemea na kusisitiza mamlaka mbalimbali kuepuka kufanya vitendo vya udhalilishaji wa Wauguzi na Wakunga.

.

Polisi yasitisha mikutano ya ndani inayofanywa na ACT-Wazalendo
Sisafiri kwenda nje kwa sababu sio jimbo langu- Rais Dkt. Magufuli