Mbunge wa Tarime vijijini kupitia Chama CHa Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, anatarajiwa kupandishwa mahakamani hii leo mara baada ya utaratibu kukamilika.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Lazaro Mambo sasa, imesema kuwa jeshi la polisi linaendelea kumshikilia mbunge huyo mpaka pale atakapopandishwa mahakamani.
Amesema kuwa sababu ya kukamatwa kwa John Heche ni zile zile walizokamatwa nazo viongozi wengine wa CHADEMA, ambao walishapandishwa mahakamani.
“Tunaendelea na utaratibu ukikamilika atapandishwa mahakamani, Heche amekamatwa kama makosa ya wenzake kina Mbowe, walitakiwa kuja sasa kwa vile hawakutokea ndio anakamatwa mmoja mmoja kama alivyokamatwa Mdee, na dhamana bado hajapatiwa bado taratibu zinaendelea”, amesema Kamanda Mambosasa.
-
Serikali yaomba kesi ya Mbowe na wenzake iende haraka
-
Magufuli aishukia Tanesco, aagiza kushusha bei ya umeme
-
Mbowe atoa neno baada ya kuachiwa huru, adai kufichua mazito
Hata hivyo, siku za hivi karibuni baadhi ya viongozi na wabunge wa CHADEMA wamekamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani, kwa tuhuma za makosa ya kufanya mandamano yasiyokuwa na kibali, na mikutano ya kisiasa.