Marais wa Uturuki, Iran na Urusi wamesema kuwa wameungana ili kuhakikisha amani inapatikana nchini Syria na kuwalinda raia wa nchi ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.
Taarifa hiyo ya pamoja ya viongozi hao, Recep Tayyip Erdogan, Vladimir Putin na Hassan Rouhani iliwekwa katika tovuti ya rais wa Iran baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika mjini Ankara nchini Uturuki.
Aidha, Viongozi hao walifanya mkutano na kila mmoja wao kwa nyakati tofauti kabla ya kuanza kwa mkutano wa pamoja ambao uliiweka kando Marekani ambayo ina vikosi vya majeshi nchini Syria.
Hata hivyo, Rais wa Iran, Hassan Rouhani ameitupia lawama Marekani kwa kuliunga mkono kundi la wanamgambo linalojiita Dola la Kiislamu nchini Syria na kutoa wito kwa nchi zote kuheshimu uhuru wa mshirika wake mkubwa katika mataifa ya kiarabu katika mashariki ya kati.
-
Marekani yalalama baada ya China kulipiza kisasi
-
Aliyekuwa Rais wa Brazil kutumikia miaka 12 jela kwa ufisadi
-
Walioathiriwa na sakata la Facebook wafika milioni 87