Mahakama imemuhukumu Rais wa zamani wa Korea kusini, anayejulikana kwa jina la Park Geun-hye kifungo cha miaka 24 jela na faini ya ($17milioni) sawa na bilioni 38 pesa ya kitanzania, kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Rais huyo ameshtakiwa baada ya kufunguliwa mashtaka 18 ya rushwa na kukutwa na hatia ya makosa mbalimbali yakiwemo, kuitukana Serikali, kuingilia baadhi ya uchaguzi na kutumia njia zisizo za halali kuchukua maoni kipindi cha uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2016, lakini pia Rais huyo anakabiliwa na tuhuma za kuvujisha baadhi ya nyaraka za siri za serikali hiyo.
Aidha Rais huyo amekana mashaka yote yanayomkabili na kudai kuwa Mahakama hiyo imekuwa ikimuonea.
Rais huyo aliondolewa madarakani mnamo mwaka 2017 kufuatia maandamano ya watu kupinga utawala wake nakutaka ajiuzulu.
Muda mchache baada ya kuondolewa madarakani alikamatwa na Polisi na kuwekwa mahabusu.