Klabu ya Bayern Munich imetwaa taji la Bundesliga msimu wa 2018/19 baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Augsburg.
Bayern sasa imeweka rekodi ya kutwaa taji hilo mara 6 mfululizo huku msimu huu wakiwa wamechukua zikiwa zimebaki mechi 5 kabla ya ligi hiyo kumalizika.
Bayern ambayo inanolewa na kocha wa muda na aliyewahi kuipa mataji matatu (Trebble), Jupp Heynckes, ilianza vibaya msimu huu chini ya kocha, Carlo Ancelotti ambaye baadae alitimuliwa na kurejeshwa kwa Jupp na kila kitu kilibadilika kuanzia hapo.
Aidha, tangu msimu wa 2012/13 Bayern haijapoteza taji hilo na imekuwa ikichukua bila ushindani mkubwa haswa baada ya mpinzani wake Borussia Dortmund kutokuwa kwenye kiwango kizuri misimu ya hivi karibuni.
-
Liverpool yaipoteza maboya Manchester City
-
Gennaro Ivan Gattuso kuinoa AC Milan hadi 2021
-
Juergen Klopp: Sitaki kumuharakisha Mo Salah