Timu ya taifa ya soka ya wanawake Twiga Stars imetupwa nje ya mashindano ya kuwania kufuzu fainali za AFCON 2018 kwa wanawake baada ya kutoa sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Zambia.
Katika mchezo huo Twiga ilijitahidi kuzuia kufungwa lakini imeponzwa na sare ya 3-3 ambayo ilipatikana kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumanne iliyopita.
Aidha, Zambia sasa imesonga mbele ambapo imebakiza mchezo mmoja ambao itacheza na mshindi kati ya Namibia na Zimbabwe na endapo itashinda basi itakuwa imekata tiketi ya kucheza fainali hizo zitakazofanyika nchini Ghana.
Hata hivyo, Twiga Stars itarejea nyumbani kujipanga tena katika awamu nyingine na michuano mingine. Tanzania sasa inawakilishwa na Ngorongoro Heroes pekee ambayo inasubiri kucheza na DR Congo kwenye mchezo wa marudiano baada ya kutoka 0-0 kwenye mechi ya kwanza.
-
Rufaa ya Wambura yagonga mwamba
-
Singida Utd yatulizwa Namfua stadium
-
Aanza safari kwa baiskeli kuelekea Urusi kushuhudia kombe la dunia