Kocha mkuu wa miamba ya soka barani Afrika, Zamalek Ihab Galal ameamua kujiuzulu nafasi yake ya kuifundisha timu hiyo kutokana na kushindwa kupata matokeo mazuri katika michezo iliyochezwa hivi karibuni.
Galal ameachia ngazi jana, Jumapili baada ya kuitumikia Zamalek kwa miezi minne na kuongoza katika michezo 16.
Aidha, Kocha huyo amejiuzuru muda mfupi baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Maqassa kwenye ligi kuu nchini Misri, huku ikiondoshwa kwenye michuano ya kombe la shirikisho baarani Afrika na Weleyta Dicha wiki chache zilizopita.
“Nimesha jiuzuru. Sito endelea kuwepo Zamalek, ni mwisho” amesema Galal.
Kocha huyo alijiunga na Zamalek mwezi Januari mwaka huu na kuchukua nafasi ya Nebojsa Jovovic na kuiongoza zamalek kushinda michezo saba kati ya 14 waliocheza kwenye ligi nchini Misri.