Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imeanza kusikiliza rufaa ambayo inapinga utaratibu uliotumika kuondoa kipengele cha ukomo wa umri kwa mgombea wa uraisi nchini humo.

Jopo la Majaji watano wanasikiliza kesi hiyo katika mahakama iliyopo Mbale eneo la kilometa 300 mashariki mwa Mji Mkuu wa Kampala.

Wabunge walipiga kura kuondolewa kwa kipengele cha umri unaozidi miaka 75 hivyo kumpa nafasi Rais aliyoko madarakani kuendelea na kugombea tena katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2021.

JPM kuwania tuzo ya kiongozi bora Afrika
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 10, 2018