Marekani, Ufaransa na Uingereza zimefanya shambulizi nchini Syria kumuadhibu rais wa nchi hiyo, Bashar al-Assad kwa shambulio la silaha za sumu dhidi ya raia na kuzuia kufanya hivyo tena.
Televisheni ya taifa nchini Syria imeripoti kuwamba vifaa vya ulinzi wa anga vya Syria, vilijibu shambulio hilo baada ya shambulio la Marekani na washirika wake kutulia.
Aidha, baada ya majibizano hayo ya mashambulizi kutulia, magari yenye vipaza sauti yaliingia katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus huku yakipiga nyimbo zinazohimiza umoja na mshikamano wa kitaifa.
Kwa upande wake, rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa Marekani itaendelea na msimamo wake wa kufanya mashambulizi dhidi ya rais Assad mpaka pale atakapoacha kuwaua raia wake kwa silaha za sumu zilizopigwa marufuku na umoja wa kimataifa.
“Shambulio la uovu na la kinyama limesababisha wakina mama baba na watoto wachanga na vijana kupoteza maisha kwa kukosa hewa, huu si ubinadamu bali ni unyama,”amesema Trump katika hotuba yake