Rapa Khaligraph Jones ameweka mkazo kwenye mpango wake wa kufanya kazi ana Jay Z ikiwa ni sehemu ya kutimiza ndoto yake.
Khaligraph amewahi kusikika kwenye nyimbo zake akidai kuwa mwaka huu akimalizika atakuwa amefanya kazi na Mfalme huyo wa Brooklyn.
Papa Jones amefunguka kwenye The Playlist ya Times FM, alisema ingawa hajawahi kumtafuta Jay Z na anajua ugumu wa kufanikisha hilo, anafanya kazi kwa nguvu zote ili siku moja ndoto yake ikitimia iwe rahisi kukubalika kwa Jigga.
“Naendelea kufanya kazi kubwa ili hata siku nikimuaproach Jay Z kwa ajili ya kazi, akisikia aseme kweli huyu jamaa ni mkali,” alisema.
Aidha, alieleza kuwa wakati ndoto yake na Jay Z ikiendelea, analo wazo la kufanya kazi na mtayarishaji wa muziki, Swizz Beatz’.
- Aliyedai kuwa ni mtoto wa Lowassa atiwa mbaroni
- Akamatwa kwa kumtupa mtoto kutoka juu ya paa la nyumba
Alisema kwa Swizz Beatz ni rahisi kuliko kumpata Jay Z, kwahiyo ana imani kubwa kuwa atafanikisha kirahisi kwa mtayarishaji huyo kwanza.
Kumpata Jay Z sio jambo dogo, DJ Khaled aliwahi kueleza kuwa ilimchukua zaidi ya mwaka mmoja, ikabidi apange nyumba kwa muda katika jiji ambalo Jigga anapatikana kirahisi, muda huo akiendelea kumshawishi kuingia kwenye project ya ‘I got the Keys’.