Moris Peter Shirima, mkazi wa Kilimanjaro, Rombo kupitia kipindi cha MKASA amefunguka jinsi alivyopata ulemavu uliopelekea mke wake aliyefunga nae ndoa kushindwa kumvumilia na kumkimbia, amefunguka juu ya mateso, karaha, shida na namna alivyokata tamaa juu ya maisha.
Kupitia MKASA ameomba msaada kwa wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wasikie kilio chake na wamsaidie kupata matibabu.
Mkasa ni kipindi kinachogusa maisha ya watu mbalimbali ambapo Dar24 inatoa fursa kwa watu hao kuzungumzia changamoto, matatizo, majanga, na mambo mengineyo mazuri na mabaya ambayo mtu ameyapitia au anayapitia, lengo likiwa ni kusaidia, kuelimisha na kufundisha juu ya maisha ambayo mwanadamu anayaishi kila siku.
Tazama Video hapa chini kusikiliza MKASA uliomkuta bwana Shirima, akimlilia Makonda, na akisimulia kinagaubaga jinsi alivyokimbiwa na mke wake mara baada ya kufikiwa na matatizo hayo.