Rais wa Angola, Joao Lourenco amemfuta kazi Mkuu wa Majeshi Jenerali Geraldo Sachipengo Nunda, baada ya kutajwa katika kashfa ya ufisadi.

Kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwezi Septemba mwaka uliopita, amekuwa akiachana na waliokuwa washirika wa rais wa zamani Jose Eduardo dos Santos aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 37.

Mnamo mwezi Novemba mwaka jana Lourenco alimfuta kazi kamanda wa jeshi la polisi Ambrosio de Lemos na mkuu wa upelelezi (usalama wa taifa), Antonio Jose Maria katika mabadiliko makubwa ya kwanza ya vyombo vya usalama tangu alipoingia madarakani mwezi Septemba mwaka jana.

Miezi michache baadae alimfuta kazi binti wa rais wa zamani Isabel Dos Santos ambaye alikuwa mkuu wa kampuni ya mafuta nchini humo na mwanamke tajiri zaidi barani Afrika kinyume na matarajio ya wengi.

 

Madaktari DRC wagoma wakiishutumu Serikali
Rais wa zamani Malawi kutoka mafichoni, Polisi wammulika