Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amelihutubia Bunge la Afrika Mashariki mkoani Dodoma na kuwapongeza wabunge hao kwa kuchaguliwa kuwa wabunge wa Afrika Mashariki.

Aidha, amewataka wabunge hao kuwatumikia wananchi wa Afrika Mashariki kwakuwa waliwachagua wakiwa na imani kuwa watawatumikia kwa uaminifu.

Amesema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki imepiga hatua kubwa katika ukuaji wa uchumi duniani ambapo amewataka wabunge hao kushikamana ili kuweza kuimarisha uchumi zaidi.

“Kwasasa tunaelekea hatua ya tatu ya ushirikiano wa kifedha, hivyo niwahakikishie kuwa tutafanya kazi kwa pamoja na nitawapa ushirikiano mkubwa,”amesema Rais Dkt. Magufuli

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 25, 2018
Kibarua cha Massimo Oddo chaota nyasi