Watu kumi na mbili wanashikiliwa kufuatia kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya ambayo leo hii inaendelea kuunguruma mahakamani.

Kufuatia kesi hiyo Mkaguzi wa Polisi, Damian Chilumba amesema kuwa wamegundua meseji ambazo alitumiwa Marehemu Msuya siku moja kabla ya kifo chake na ujumbe mwingine aliotumiwa saa chache kabla ya kifo chake akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Taifa, Kilimanjaro International Airport (KIA).

Chilumba amesema siku moja kabla ya tukio hilo namba ya Airtell iliyosajiliwa kwa jina la Motii Mongululu ilimtumia ujumbe Biolionea Msuya ikimwambia ”Nina Riziki” na siku ya tukio la kifo chake namba ile ile ilimuandikia tena ”Niko KIA nakusubiri hapa”.

Aidha Bilionea Erasto Msuya alifariki dunia mnamo Agosti 7, 2013 kwa kupigwa risasi 22 karibu na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

 

Mrithi wa Lwandamina apatikana DRC
Nikki wa pili: Unyonge wa nini?