Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo Aprili 26, 2018, amepokea msaada kutoka kwa taasisi mbili tofauti za Zanzibar; Abdullah Aid Emergency Appeal na Darul Irshad Islamic Centre kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko waliopoteza mali zao hivi karibuni kutokana na mvua zilizonyesha mfululizo kwa zaidi ya siku tatu.

Misaada iliyotolewa ni pamoja na Magodoro, Chandarua, Mashuka, Mito, Sukari, Unga, Mchele pamoja na Mafuta ya kupikia.

RC Makonda amesema misaada hiyo itagawanywa kwa familia zaidi ya 600 zilizoathiriwa na mafuriko lengo likiwa ni kusaidia familia hizo ambazo zimekuwa zikiishi kwa tabu baada ya mvua kuharibu vyakula na mali.

Aidha RC Makonda amezishukuru taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center kwa kuamua kutumia maadhimisho ya muungano kugusa maisha ya familia zilizokuwa zikiishi kwa tabu.

Pia RC Makonda amesema kuwa Mkoa umeandaa mkakati wa kukabiliana na mafuriko ya mara kwa mara ambapo hivi karibuni ataitisha mkutano na wananchi wote waishio mabondeni ili kuangalia namna bora kutatua suala hilo.

 

Zlatan Ibrahimovic hatokwenda Urusi
Kamati ya saa 72 yaangusha rungu la adhabu