Wananchi pamoja na viongozi wa Serikali wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Wameungana na Watanzania wenzao nchini kusheherekea miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya usafi maeneo mbalimbali ikiwemo hospital ya Ilembula pamoja na mitaani.
 
Katika sherehe hizo mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Ally Kassinge amewataka wananchi hao kuuenzi muungano kwa kudumisha amani na Upendo baina yao ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima
 
“Tuuenzi muungano wetu kwa kuitunza amani tuliyonayo kwa faida ya familia na jamii zetu kwa ujumla,” amesema Kassinge.
Hata hivyo katika sherehe hizo pia mkuu wa wilaya hiyo amezindua chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ambapo amesema zaidi ya wasichana 1000 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo.
 
Kwa upande wa mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya wanging’ombe, James Ligwa,amesema kuwa zaidi ya wanawake 500 wamepimwa kwa kipindi cha miezi minne ambapo 50 kati yao wamegundulika kuwa na dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi.

Video: Jinsi Polisi walivyozima maandamano, JPM aduwaza
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 27, 2018