Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.