Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita anatarajia kuungana na mashabiki wa soka hapa nchini kushuhudia mtanange kati ya watani wa jadi Simba na Yanga.
Katika mchezo huo ambao mashabiki wa timu zote mbili wamekuwa wakitupiana tambo za ushindi, unatarajiwa kuchezwa leo katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Aidha, Mwita ataungana pia na viongozi mbalimbali ambao watahudhuria kushuhudia mtanange huo akiwemo mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na wabunge mbalimbali.
Hata hivyo, katika mchezo huo Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.