Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma, amesema kuwa kivutio kikubwa kwa wasanii wa kike ni nguo zenye mpasuo kwani wakivaa madera kwenye nyimbo zao na filamu wanazotengeneza hawatapata wateja wa kazi zao.
Amesema kuwa wanatakiwa kupewa elimu maalum na si kuwafungia kwasababu wakiwafungia wanaua vipaji vyao na kuwadidimiza kisanaa.
Aidha, Msukuma ameongeza kuwa wasanii hao wanalitangaza taifa kimataifa, tofauti na serikali ilikowekeza nguvu nyingi kwenye michezo mingine kama mpira wa miguu ambao umekuwa haufanyi vizuri.
“Msanii anafanya kazi nzuri kwenye amerekodi akikosea tu kidogo mpasuo Waziri huyo amefungia, sasa mimi nataka kumuuliza, unafungia miziki ya Tanzania, unawafungia wasanii wa Tanzania kuoynesha mpasuo, hebu angalia miziki ya kina Rihana, na ndio mnakaa mnaangalia kwenye YouTube humu kila siku, hii ya Tanzania mnataka wasanii wetu wavae dera sijui wavae pekosi, hakuna mtu ana hobi ya miziki ya pekosi miaka hii ya sasa, msanii anafanya kazi nzuri, anawekeza pesa ya mkopo, akikosea kidogo mnafunga,”amesema Msukuma