Kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, imepinga kitendo cha serikali kuhamisha baadhi ya walimu wa shule za Sekondari kwenda kufundisha shule elimu ngazi ya msingi.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, alipokuwa akimuwakilisha mwenyekiti wa kamati hiyo Peter Serukamba, wakati wa kuwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 2018/2019, na kuomba serikali kuzingatia kwa makini uamuzi huo kwani hepelekea kupunguza morali kwa walimu.

“Kamati inaona kitendo cha kuwachukua walimu wa sekondari kwenda kufundisha shule za msingi sio sawa kwakuwa kila ngazi ya ualimu inamiongozo na mafunzo yake mahususi,”amesema Bashe

Aidha, taarifa ya kamati hiyo imesema kuwa kumchukua mwalimu wa sekondari kufundisha elimu ya msingi imepokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa jamii na walimu wenyewe ikiwemo hisia za kushusha morali ya kufanyakazi.

Hata hivyo, kwa upande mwingine kamati hiyo ya kudumu ya Bunge imeshauri serikali kuunda bodi ya taaluma ya walimu ambayo itakua na jukumu la kufuatilia ubora wa elimu inayotolewa nchini.

 

 

 

 

 

Sakata la Nondo laibuliwa Bungeni, ''Umekitia aibu chuo''
Video: Lissu nimesahau kutembea, Mabilioni yayeyuka