Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Ajira na
watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama ameweka jiwe la msingi katika jengo la
kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
linalojengwa katika Halimashauri ya Wilaya ya Simanjaro ,Mkaoani Manyara kwa
ufadhili wa Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI ATF kwa kushirikiana na
halmashauri.
Akiweka jiwe la msingi, Mhagama amesema kuwa Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti
UKIMWI (ATF) umechangia Shilingi milioni mia mbili na halimashauri ya Simanjiro
imechangia Shilingi milioni 51,599,533.
Aidha, Mhagama amefafanua kuwa kwa ujumla Mradi huo utagharimu jumla ya Sh
251,599,593 na unajengwa katika awamu mbili. Awamu ya kwanza yenye vyumba vya
mapokezi, kumbukumbu, vyumba viwili vya ushauri nasaha, vyumba viwili vya Madaktari,
sehemu ya kusubiria, sehemu ya kutolea dawa, stoo ya dawa, chumba cha kifua kikuu
na stoo ya kuhifadhia vifaa vya usafi.
-
Video: Magufuli azindua daraja jipya lililopewa jina lake
-
TAMISEMI yawaonya wanaombeza Makonda
-
Sirro kuzindua kombe Kibiti
Hata hivyo, awamu ya pili ya mradi huo itagharimu Shs. 240,400,467/= na itajumuisha
vyumba vya maabara, chumba cha mionzi, chumba za USS, Vyoo na sehemu ya
kusubiria.