Yapata mwaka sasa tangu taifa lilipokumbwa na msiba mkubwa siku kama ya leo Mei 6, 2018 ambapo tulipoteza wanafunzi 32 wa darasa la saba, dereva na mwalimu mmoja toka shule ya msingi Lucky Vincent waliokuwa wakitokea jijini Arusha kueleka Karatu kwa ajili ya mitihani ya kujipima uwezo.
Ajali hiyo ilitokea mara baada ya dereva wa gari aina ya Coaster kudaiwa kushindwa kulimudu na kutumbukia kwenye korongo mida ya saa mbili asubuhi katika eneo la Mto Marera.
Aidha Shule ya Msingi Lucky Vincent anaadhimisha siku hii ya leo kwa kufanya misa takatifu ya kuwaombea marehemu wote waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
Misa hiyo imehudhuriwa na watoto watatu walionusurika kufa katika ajali hiyo ambao ni, Saida Awadh, Wilson Tarimo na Doreen Mshana.
Msiba huo uligusa taifa kwa ujumla kutokana kifo cha ghafla cha wanafunzi hao, Mungu azipumzishe roho za marehemu wote kwa amani.
Kilio kilitawala kwa watanzania wote viongozi mbalimbali walihudhuria katika viwanja vya Aman Abeid Karume, jijini Arusha eneo ambalo lilitumika kuaga miili ya wanafunzi hao na kuikabidhi kwa familia zao.