Viongozi wa mataifa ya Ulaya wamesema kuwa wataendelea kuunga mkono makubaliano ya Kinyuklia ya Iran baada ya Marekani kutangaza kuwa imejiondoa katika makubaliano hayo.
Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimesema kuwa zitaendelea kuwa katika mkataba huo na pia kufanya kazi na mataifa yote, hivyo wameitaka Marekani kutovuruga utekelezwaji wake.
Aidha, mataifa mengine yalioweka mkataba huo wa 2015- Urusi na China pia yamesema yataendelea kuunga mkono makubaliano hayo.
“Mataifa yetu yataendelea kuunga mkono makubaliano hayo na yatafanya kazi na mataifa yanaoendelea kuunga mkono mkataba huo,” Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zimesema katika taarifa ya pamoja.
Hata hivyo, Iran imesema kuwa inafanya kazi ya kunusuru makubaliano hayo bila ya ushirikiano wa Marekani.
-
Israel yaapa kuishughulikia Iran
-
Israel, Saudi Arabia zampongeza Trump, Iran yamuonya
-
Iran yamtahadharisha Trump kuhusu mkataba