Watu waliojihami kwa mabomu ya kujitoa mhanga wamelipua makanisa matatu katika jiji la Surabaya nchini Indonesia na kuua watu 11.
Imeelezwa kuwa karibu watu 40 walijeruhiwa vibaya kutokana na shambulio hilo lilitokea ndani ya dakika chache za mlipuko wa kanisa la kwanza, lakini hadi sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na tukio hilo.
Aidha, Afisa wa kitengo cha ujasusi cha Indonesia, Wawan Purwanto, amesema kuwa kundi la Jemaah Ansharut Daulah (JAD) lenye ushirika na kundi la kigaidi la Islamic State linahusishwa na tukio hilo.
Amesema kuwa tukio hilo lina uhusiano na tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa askari watano wa jeshi la polisi, walipokuwa waawahamisha wafungwa magaidi katika moja ya gereza lenye ulinzi mkali zaidi nchini humo katika jiji la Jakarta.
Zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Indonesia ni waumini wa dini ya Kiislamu huku asilimia chache zikiwa na waamini wa imani ya Hindu, Kikristo na Buddha.
Barua ya maombi ya kazi itakayomshika muajiri wako
Shambulizi hilo linatajwa kuwa shambulizi baya zaidi la kigaidi tangu mwaka 2005 ambapo mashambulizi matatu ya kujitoa mhanga yalisababisha vifo vya watu 20 nchini humo.