Kikosi cha Timu ya Taifa ya Nigeria kinaingia nchini Urusi kulisaka Kombe la Dunia linalotolewa na Fifa, ikiwa imepangwa kwenye kundi D ikiwa pamoja na Argentina, Iceland na Croatia.

Nigeria ilifuzu fainali za kombe la dunia 2018, ikitokea ukanda wa bara la Afrika (CAF), kwa kuzibwaga timu za taifa za Algeria, Cameroon na mabingwa wa bara hilo mwaka 2012 Zambia.

Nigeria ilimaliza nafasi ya kwanza kundi B (kundi la pili), kwa kufikisha alama 13, ikifuatiwa na Zambia waliokuwa na alama 8, Cameroon ilishika nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 7 na Algeria iliburuza mkia kwa kupata alama 4.

Jina la utani la timu ya taifa ya Nigeria: Super Eagles

Mfumo: Kikosi cha Nigeria hutumia mfumo wa 4-3-3.

Image result for Victor Moses - nigeriaMchezaji Nyota: Victor Moses (Chelsea)

Image result for Alex Iwobi - nigeriaMchezaji hatari: Alex Iwobi (Arsenal).

Image result for John Obi Mikel - nigeriaNahodha: John Obi Mikel (Tianjin TEDA)

Image result for Gernot Rohr - nigeriaKocha: Gernot Rohr (64), raia wa Ujerumani.

Ushiriki: Nigeria imeshiriki fainali za kombe la dunia mara tano (5). Mwaka 1994, 1998, 2002, 2010 na 2014

Mafanikio: Hatua ya mtoano (16 bora 1994 na 2014)

 

Kuelekea 2018:

Ujio wa kocha Gernot Rohr aliechukuwa nafasi ya mzawa Sunday Oliseh, ilionesha kuibua hamasa kwa wachezaji pamoja na mashabiki wakati wa kuwania kufuzu fainali za

2018.

Kocha Rohr alijitahidi kuifanya kazi yake vyema, na wakati mwingine alitumia muda wake kukaa na mchezaji mmoja mmoja walipokuwa kambini na kumueleza nini wanachostahili kukifanya katika michezo ya kuwania kufuzu.

Zoezi la kuwa karibu na wachezaji lilifanikiwa na kuiwezesha Nigeria kuwa taifa la kwanza barani Afrika kukata tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia 2018.

Kocha huyo ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha klabu ya Bordeaux ya Ufaransa alipoteza mchezo mmoja pekee, wakati wa kuwania kufuzu kwa kukubali kufungwa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Algeria waliokuwa kwao Stade Mohamed Hamlaoui, mjini Constantine Novemba 10, 2017.

Kukomaa kwa Alex Iwobi wa Arsenal na uzoefu wa mshambuliaji wa pembeni Victor Moses wa Chelsea, unampa ujasiri mkubwa kocha huyo kuelekea katika fainali za kombe la dunia.

Nigeria wataanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Croatia, Uwanja Kaliningrad, mjini Kaliningrad Juni 16, kisha watapambana na Iceland Juni 21, Uwanja wa Volgograd, mjini Volgograd, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watakutana na Argentina Juni 26, Uwanja Krestovsky, mjini Saint Petersburg.

Gernot Rohr ametamba kuwa kikosi chake kitaishangaza dunia kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu. Afrika tunashawishika kuweka imani yetu kwenye kikosi hiki na kusubiri kuona matokeo kama tutang’ara kwenye mashindano hayo.

Tumekamilisha kundi D, kesho tunaanza kuzimulika timu za kundi E, zikiwa zimebaki siku 14 tu kuanza kushuhudia mtanange huo.

Endelea kukaa hapa na Dar24, fuatilia YouTube Channel yetu ya Dar24 Media kupata mengi zaidi kuhusu Fainali za Kombe la Dunia, Burudani, Siasa na Maisha.

Singida United yatambulisha silaha mpya
Tafiti: Kila baada ya sekunde 6 watumiaji wa tumbaku hufariki dunia