Siku moja baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema amepeleka ombi kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutaka kuundwa kwa sheria ya kuruhusu mtu kujipima Virusi vya Ukimwi suala hilo limezua sura tofauti kwa watu tofauti tofauti wakiwemo wataalamu wa Afya.
Baadhi wanapinga mpango huo kwa hoja kuwa una madhara kulinganisha na faida na wengine wakisema iwapi miongozo itafuatwa utakuwa na manufaa.
Moja ya madaktari amesema kufanya hivyo ni kazi bure kwa kuwa anaweza kwenda hospitali kuanza dawa au kuamua kulipiza kisasi kwa anaodhani wamemwambukiza.
Mkurugenzi wa TACAIDS, Leonard Maboko amesema utaratibu mzuri wa mpango huo utaongeza ari ya watu kutambua afya zao kwani kuna watu ambao wanapenda kujua afya zao ila wanaogopa kwenda hospitali na zahanati hivyo hiyo ni fursa kwao kutumia njia hii kutambu afya zao.
-
Video: Polisi watanda, Dkt Bashiru aanza kubadili mwelekeo.
-
Waziri wa Elimu avurugwa na Kwaya ya Utupu ya Wanafunzi
Mwalimu ambaye pia anahusika na maendeleo ya jamii na wazee alisema hayo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Mtambulie CUF Masoud Abdalla Salim alipohoji juu ya mikakati ya serikali juu ya kuwatambua wale wanaopata Ukimwi.
Ambapo Ummy alijibu tayari wamewasilisha ombi kwa Mwanasheria mkuu kupitisha sheria ili mtu aweze kujipima mwenyewe ugonjwa huo.
Ambapo kwa kutumia kipimo hiko kitamwezesha mtu kujua hali yake ndani ya dakika 15 hivyo itasaidia kupambana dhidi ya ugonjwa huo kwa kuanza kuchukua hatua mapema.
Je nini maoni yako juu ya swala hili, unaunga mkono hoja ya Ummy Mwalimu ya mtu kujipimwa mwenyewe Ukimwi akiwa nyumbani?