Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee amesema kuwa anaona aibu kubwa kuwa mwanafunzi wa Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kwasababu ameshindwa kuliambia bunge zilikopotelea shil. 424 trilioni  ambazo serikali ilidai italipwa na Mgodi wa Acacia kama kodi waliyokwepa kuilipa.

Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ya mwaka 2018/ 19 ambapo amesema kuwa Prof. Kabudi amesema kuwa hawatasema kiasi kilichopangwa kutolewa na makampuni hayo.

“Tuliwahi kusema kuwa shida si Acacia, shida ni serikali, naona aibu kubwa kusema kuwa Prof. Kabudi ni mwalimu wangu, Waziri anasema kuwa hawezi kutaja kiasi gani kimelipwa, kwasababu kuna watu watakuja wanaotudai,”amesema Mdee

Hata hivyo, Mdee alikataliwa kutoa taarifa na wabunge wa CCM na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama.

 

 

Suti ya Sugu yazua utata Bungeni
Mbunge wa CCM awafananisha wapinzani na Mbwa