Kampuni ya Ndege ya Emirates imezindua ndege ambayo imetengenezwa na madirisha bandia hivyo abiria watakuwa wakiona nje kwa kutumia Kamera maalumu zilizofungwa katika ndege hiyo.
Kampuni hiyo imesema kuwa hatua hiyo inatoa fursa ya kuondoa madirisha yote katika ndege za siku zijazo, suala litakalozifanya kuwa nyepesi na kuongeza kasi yake.
Aidha, Rais wa Emirates, Sir Tim Clark amesema kuwa mfumo huo wa kutumia Kamera utakuwa ni mzuri zaidi kuliko ule wa awali ambao unatazamwa kwa macho.
Hata hivyo maafisa wa usalama wa anga kutoka mamlaka ya kudhitibi anga barani Ulaya European Aviation Safety Agency wamesema kuwa hawaoni changamoto yeyote kuhusu ndege ambazo hazina madirisha.