Viongozi wa dini Wilayani Ilala Jijini Dar es salaam wametakiwa kusaidia katika kufundisha maadili mema kwa watoto ili wabaki na tamaduni za kitanzania na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi hao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakati akitoa neno la shukrani katika Futari aliyoiandaa kwa ajili ya Watoto yatima wa wilaya hiyo.

“Viongozi wetu wa dini tunataka tuwatumie kunapokuwa na mambo magumu, tutaendelea kushirikiana nanyi katika yote tunayoyafanya, masuala ya imani yanahitajika sana na ninyi ndiyo kazi yenu kubwa, ushirikiano huu hautaishia kwenye Futari tu,”amesema DC Mjema

Aidha amewataka wananchi kuitunza amani ya nchi na kuwataka kufanya kazi kwa bidii ili kuijenga nchi na ikiwa kuna jambo ambalo haliendi sawa wasisite kutoa ushauri kwa viongozi wao ili kuendeleza amani na umoja wa kitaifa.

Hata hivyo, kwa upande wake Sheikh wa Wilaya ya Ilala, Adam Mwinyipingu amewataka Waislam kuzingatia maagizo ya viongozi wao katika kuswali swala ya Eid itakayo swaliwa kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 15, 2018
Pato la Taifa lazidi kuongezeka