Walid, msanii wa Tanzania ambaye yuko chini ya usimamizi wa mwaamuziki Patoranking wa Nigeria, amefunguka jinsi ambavyo kaseti yenye wimbo wa Mr. Ebo ilivyobadili maisha yake kimuziki.
Mkali huyo wa ‘Namna Gani’ ambaye amekulia nchini Uholanzi hadi alipofikia umri wa miaka 13, amefunguka kwenye mahojiano maalum na Dar24 katika ofisi za kampuni hiyo inayotoa ‘Taarifa Bila Mipaka’, kuwa siku moja akiwa amerejea Bongo alibaini kaseti yenye nyimbo kadhaa za muziki wa Afrika Mashariki, lakini wimbo wa marehemu Mr. Ebo ‘Mi Masai’ ndio uliobadili mengi.
Walid anayefanya vizuri na ngoma zake ‘Namna Gani, Dunia na Ni Wewe’ aliomshirikisha Bosi wake, Patoranking amesema ilikuwa mwaka 2003 akiwa na umri mdogo, alipovutwa na wimbo huo wa Mr. Ebo na kuanza kuifuatilia Bongo Fleva hali iliyosababisha leo ni msanii mkubwa aliyelenga kunasa pia soko la Bongo.
Uswisi wafunguka walivyompania Neymar leo
“Nilivyokipiga [kikaseti] nikakuta nyimbo za Afrika Mashariki kama nyimbo za Redson… Mr. Ebo alikuwepo pia na wimbo wake ‘Mi Mmasai’ na huo ndio wimbo uliochukua attention yangu, sasa kuanzia hapo nikawa nafuatilia Bongo Fleva,” alifunguka.
Angalia mahojiano yote hapa, ufahamu anachofanya na Nandy, alivyonaswa na Pantoranking na mengine mengi: