Leo June 26, 2018 Bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge la Jahmuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema endapo wabunge wataipigia kura ya Hapana bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/2019 Rais atalivunja Bunge, maelezo hayo ni kufutia kikao kinachofanyika muda huu cha kuipitisha bajeti hiyo.
”Endapo mlio wengi mtaikataa Bajeti ya Serikali, Bunge hili Rais atalivunja haraka na baadhi yenu mkirudishwa majimboni hamrudi kwa hiyo akili za kuambiwa changanya na zako ” amesema Ndugai.
Aidha amewaomba wabunge wote kuwapo bungeni huku akisistiza kwamba mbunge hapigi kura kwa jambo moja, bali ni kwa mfuko wote wa bajeti, kwa hiyo ni vizuri wananchi wakaelewa.
Kufuatia kauli hiyo iliyotolewa na Spika Ndugai imemuibua Mbunge wa Kawe, Halima Mdee aliyetumia ukurasa wake wa Twitter na kutoa maoni yake akisema hakuna shida yeyote endapo bunge likavunjwa kwa kusimamia Serikali.
” Hili ndio Bunge la Tanzania na huyu ndiye kiongozi wa Mhimili” na kumalizia Hivi Bunge likivunjwa kwa kusimamia Serikali shida iko wapi” amehoji Mdee..
Aidha matangazo ya upigaji kura ya wazi kwa ajili ya kupitisha bajeti ya kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019 yanarushwa mubashara na vituo mbalimbali vya televisheni nchini ikiwemo Televisheni ya taifa TBC.