Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amemuagiza Mbunge wa Mikumi (CHADEMA) Joseph Haule ‘Prof. Jay’, kupeleka ushahidi kutokana na kuwa na madai ya kupotea watu 40 katika kata ya Luhembe, jimboni kwake.
Hasunga ametoa agizo hilo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mikumi lililohoji, kuwa anaomba ufafanuzi kwa serikali juu ya kupotea kwa watu 40 jimboni kwake na hawajulikani walipo na tabia ya watumishi wa TANAPA kuwachukua wakazi wa Mikumi na kuwatesa.
“Mheshimiwa Mbunge naomba ulete ushahidi wa kupotea kwa wananchi ili kutanabaisha taarifa hizo na serikali itashughulikia suala hilo maana serikali ipo kwa kulinda usalama wa wananchi,”
Hata hivyo, Naibu Waziri ameongeza kuwa serikali tayari imetatua mgogoro wa mpaka kati ya wakazi wa Mikumi na maeneo ya hifadhi.
-
Hatma ya Mbowe na wenzake kujulikana julai 2 mwaka huu
-
Mwarabu Fighter amvuruga Zola D, ‘mimi ni mwalimu wako’
-
Ridhiwani: Mambo yamebadilika, sio kama enzi za JK (Video)