Mwanamitindo maarufu hapa nchini, Hamissa Mobetto ameamua kujiingiza katika sanaa ya muziki mara baada ya muda mchache kuachia ngoma inayoenda kwa jina la ”Madam hero”, ambayo ameongelea maisha yake akiamini katika kutoa tabasamu kwa jamii inayomzunguka hasa wama na wadada.
Imekuwa ”suprise” kubwa kwa mashabiki wa mwanamitindo huyo kwani imezoeleka akionekana kupamba video za wanamuziki mbalimbali ikiwemo Diamond Platinumz.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hamisa Mobetto amewaomba mashabiki wake kufutilia chaneli yake mpya ya You Tube ili waweze kuwa wakwanza kusikiliza ngoma hiyo mpya na kutaarifu kuwa siku za karibuni ataachia video ya wimbo huo.
Bado haijafahamika wazi kama mwanamitindo huyo ameamua kujikita kwenye muziki au vipi.
Bofya hapa kusikiliza kionjo cha wimbo huo, Madam Hero.