Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na kumteua Mbunge wa Mwibara, Kangi Rugola kuchukua nafasi hiyo.

Aidha Rais Magufuli amefanya teuzi nyingine ambapo amemteua Musa Ramadhani Sima kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,

Omary Mgumba kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji,

Mhandisi Isack Kamwelwe kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,

Na Athumani Kihami kuwa Katibu wa Uchaguzi NEC.

Waziri Mbarawa amehamishiwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji akitokea Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Video: Watu 20 wamefariki dunia na wengine 45 kujeruhiwa katika ajali ya magari manne Mbeya
Ajali mbaya yatokea Mbeya ikihusisha Lori na Hiace tatu za abiria