Ajali hiyo imetokea leo Julai Mosi, 2018 ambapo imehusisha magari manne zikiwamo daladala tatu za abiria na lori moja.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo mara baada ya kazi ya uokoaji kukamilika, ambapo uokoaji ulishirikisha vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Wananchi pia wameshirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika uokoaji pamoja na kunasua moja kati ya daladala hizo iliyokuwa imelaliwa na lori.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alikuwapo pia katika eneo la tukio katika uokoaji.
Lori liliyagonga magari hayo yaliyokuwa yakitokea stendi ya Mbalizi kuelekea Mbeya mjini.