Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinapinga vikali kauli iliyotolewa na Waziri wa Manbo ya Ndani, Kangi Lugola jumamosi ya tarehe 21, julai mwaka huu juu ya kutomfikisha mahakamani mshtakiwa mpaka awe amelazwa mahabusu.
LHRC imesema kauli hiyo inakiuka miongozo ya kikatiba inayoweka misingi ya dhamana pamoja na dhana ya kutokuwa na hatia mpaka pale itakapothibitika (Presumption of Innocence).
Wameongezea kuwa kitendo hiko kinaweka mazingira magumu mtuhumiwa kufikia haki ya kupata dhamana kama haki yake kikatiba kwa mujibu wa Ibara ya 13 (6) (b) cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
-
Waziri Mkuu Lee Nak-yon wa Jamhuri ya Korea amemaliza ziara yake nchini
-
Watano wahukumiwa kunyongwa kesi ya Msuya
Hali inayopelekea mshtakiwa kucheleweshewa haki au kukosa haki ya dhamana kabisa.
Hayo yameibuliwa siku chache mara baada ya Lugola kutoa agizo la kuwaweka mahabusu na kuwapandisha mahakamani madereva pamoja na wamiliki wa magari ambayo yatakuwa yamepata ajali iliyosababishwa na ubovu wa gari.