Nchini Kenya Katibu Mkuu wa Chama cha FORD, David Eseli Simiyu amesema National Super Alliance (NASA) ilisambaratika mara tu baada ya uchaguzi mkuu 2017.

Ameongezea kuwa Chama cha FORD kilikuwa bado sehemu ya muungano huo kwa sababu ya mkataba waliotia sahihi uliwaunganisha na NASA na amethibitisha kwamba muungano wa National Super Alliance (NASA) ulifariki zamani na kuzikwa siku chache baada ya Uchaguzi Mkuu, Agosti 2017.

Akizungumza na chombo cha habari cha TUKO.co.ke, Mbunge huyo wa Tongaren alisema NASA imegeuzwa kuwa Orange Democratic Movement (ODM) badala yake na ameongezea kuwa kama wasingekuwa wametia sahihi mkataba uliounganisha vyama hivyo vitatu katika NASA chama chake kingekuwa kimehama muungano wa NASA.

“Tangu 2017, viongozi wa NASA hawajawahi kukutana, mkutano wa mwisho baina ya maafisa wa NASA ulifanyika siku chache tu baada ya Uchaguzi Mkuu,” Tunaweza vipi kusema NASA bado ipo?” aliuliza.

Isitoshe, Simiyu alielezea kutotosheka kwa chama chake akisema chama kinachoongozwa na Raila kimekuwa kikifanya maamuzi kwa niaba ya NASA hata pasipo kujadiliana na vyama vingine katika mwavuli wa NASA.

“ODM ndiyo inayofanya maamuzi ilhali inahadaa umma na wafuasi wa NASA kwamba maamuzi yamejadiliwa na vyama vingine,”

“ODM imekuwa ikitawala ni nani atakayechukua nafasi katika Bunge na Seneti,” alisema

Katibu Mkuu wa Ford Kenya pia alithibitisha hatua ya kutwaa nafasi ya Seneta wa Bungoma Moses Wetangula na kumpa mwenzake wa Siaya James Orengo na kusema kwamba wao hawakufahamu mipango ya kutoa nafasi hizo.

Tanesco yazigeukia Taasisi za Serikali, sasa Polisi kulala Gizani
Muna Love awapa moyo wanaopitia magumu