Beki wa kati wa klabu ya Everton Ashley Williams amejiunga na klabu ya Stoke city kwa mkopo wa muda mrefu, baada ya pande hizo mbili kufikia makubaliano usiku wa kuamkia leo.
Beki huyo kutoka nchini Wales anajiunga na Stoke City itakayoshiriki ligi daraja la kwanza msimu wa 2018/19, kwa hitaji la kurejesha kiwango chake na kuisaidia klabu hiyo kufanikisha safari ya kurejea ligi kuu msimu ujao wa 2019/20.
Williams anaondoka Goodison Park baada ya kuitumikia The Toffees katika michezo 60 kwa kipindi cha misimu miwili aliyokuwepo klabuni hapo, huku mara ya mwisho kuonekana kikosini ilikua mwezi Machi mwaka huu.
“Kabla sijafanya maamuzi ya kujiunga na Stoke City, nilipata wakati mgumu kutafakari safari hii ya kuodnoka ligi kuu na kuja ligi daraja la kwanza, lakini nimeamua kutokana na kutambua soka linachezwa popote, na lengo la kuja hapa ni kuhakikisha ninapambana kujisaidia binafsi na kuisadia klabu hii,” Alisema Williams kumwabia mwandishi wa habari wa Tovuti ya Stoke City.
Meneja wa klabu ya Stoke Gary Rowett amekiri kufurahishwa na ujio wa beki huyo, na anaamini ataweza kufanikisha malengo aliyojiwekea huko West Midlands, ya kupambana vilivyo msimu huu ili wafanikishe kurejea ligi kuu.
“Nimezungumza na Ashley na amekiri wazi yupo tayari kupambana na kuiwezehaa klabu hii kuwa sehemu klabu zitakazofanikiwa mwishoni mwa msimu huu kwa kushirikina na wachezaji wengine,” Alisema Rowett.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 33,anakua mchezaji wasita kusajiliwa na Stoke Coty katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi, akitanguliwa na Benik Afobe, Peter Etebo, James McClean, Tom Ince na Adam Federici.
Stoke City wataanza kampeni ya kuhakikisha wanarejea ligi kuu msimu ujao, kwa kucheza na Leeds United siku ya Jumapili.