Shirikisho la soka barani Afrika limeipokonya Ghana haki za kuandaa michuano ya soka ya wanawake kwa mataifa ya Afrika (AWCON) iliyokuwa imemepangwa kuanza kufanyika miezi mitatu ijayo.
Ghana imepokwa nafasi hiyo kutokana na maandalizi ya kuandaa michuano hiyo kutoridhisha huku miezi michache ikiwa imesalia kabla ya mataifa nane kuchuana kutafuta bingwa ambaye ataungana na mshindi wa pili na watatu kuwakilisha Afrika kwenye michuano ya Kombe la dunia,Ufaransa 2019.
Aidha, Timu ya ukaguzi kutoka CAF inadaiwa kutembelee Ghana mwezi uliopita na kugundua moja kati ya viwanja vilivyopangwa kusimamia michuano hiyo havijakamlika, licha ya ujenzi kunaendelea huenda viwanja hivyo visiwe tayari wakati michuano hiyo itakapo anza kufanyika Novemba 17 hadi Desemba 1, 2018.
Wakati huo huo, Rais wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad, amedhibisha kuwa michuano hiyo itahamishiwa kwenye nchi nyingine inayotarajiwa kutajwa mwezi ujao kwenye kikao cha shirikisho hilo kitakachofanyika nchini Misri.
Mataifa nane yaliyofunzu kushiriki michuano hiyo ni pamoja na bingwa mtetezi Nigeria, Algeria, Cameroon, Equatorial Guinea, Mali, Afrika Kusini, Zambia na aliyekuwa mwenyeji Ghana.