Belcalis Marlenis Almanzar maarufu kama Cardi B amemjibu rapa Nicki Minaj kwa staili ya aina yake kupitia ukurasa wake wa instagram.

Bifu kati ya Nicki Minaj na Cardi B lilianza mara baada ya marapa hao kushirikishwa na kundi maarufu la muziki wa Trap Migos katika wimbo wa Motorsports.

Baaada ya maigizo hayo kuendelea Nicki Minaj amezungumza na vyombo vya habari vya nchini Marekani na kuthibitisha kuwa hana ugomvi na Cardi B na kumpongeza kwa mafanikio aliyofikia.

Mara baada ya rapa Card B kujifungua alianza kurusha video ambazo zilikuwa zikionesha anamponda msanii fulani japo hakumtaja.

Siku ya maadhimisho ya mitindo yanayofanyika nchini Marekani kila wiki katika jiji la NewYork linalojulikana kama Harper Bazaar ICONS rapa Cardi B alionekana akimvamia Nick Minaji na kumrushia viatu.

Nicki Mnaji alipohojiwa amesema kuwa tukio hilo ni la udhalilishaji kwa wote wawili.

“Siwezi kuzungumzia malezi ya mtu, inanishangaza jinsi watu wanavyopenda kunifanya mimi ndio nionekane mbaya, nimeona ile video iliyovuja lakini mimi nitaonekana mpumbavu” Amesema Nick Minaj.

“Umenikuta kwenye muziki, sijawahi kutembea na DJ ili wapige ngoma zangu” aliongezea Nick Minaj.

Cardi B wiki hii naye ameamsha mambo baada ya kujibu mapigo kwa kupost orodha ya wasanii waliouza albam zao kwa wingi zaidi mwaka 2018 huku katika orodha hiyo hakuiweka albam ya Nicki Minaj ya ‘Invasion Of Privacy’ na ‘Queen’ huku akiandika chini ya post hiyo kuwa namba hazidanganyi.

 

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 15, 2018
Video: Miaka mitatu ya JPM imeibua ari ya utendaji kazi- Majaliwa