Mwili wa mwandishi maarufu kutoka Tanzania, Isaack Mayenjwa Gamba aliyekuwa anafanyia kazi Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (DW) umewasili nchini tayari na shughuli ya kuuaga imeanza rasmi katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam.
Mara baada ya ibada hiyo mwili huo utapelekwa uwanja wa ndege kwa ajili ya kuusafirisha kuupeleka Bunda, Musoma kwa ajili ya mazishi.
Bi Schmidt amesema pengo la Isack haliwezi kuzibika kwani alikuwa mchapa kazi, mbunifu mcheshi na asiyekata tamaa
”Nakumbuka wakati mmoja kabla ya kuja Tanzania alisema naenda nyumbani kula bata akiwa na maana kwamba kufurahia maisha,” amesema.
Mwandishi huyo, aliyekuwa mtangazaji wa michezo na burudani katika DW alipatikana akiwa amefariki dunia mjini Bonn nchini Ujerumani Alhamisi ya tarehe 18 Oktoba baada ya kutoonekana afisini Jumanne na Jumatano.
Kutoonekana kwake kazini kuliwashtua wafanyakazi wenzake, na kuwafanya waamue kwenda kutoa taarifa polisi ambao walifika nyumbani kwake na kuvunja mlango uliokuwa umefungwa na kumkuta amefariki dunia.