Mamlaka ya kudhibiti Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA imeamua kumfungulia kesi msanii wa filamu nchini Wema Sepetu mara baada ya kumkuta na kosa la kuchapisha na kusambaza maudhui ya ngono mtandaoni.

Shitaka hilo lilifunguliwa jalada la kesi namba KJN/ RB/13607/2018-kuchapisha na kusambaza maudhui ya ngono mtandaoni.

Kesi hiyo imefunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar.

Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, endapo itathibitika kwamba kweli msaanii huyo ana hatia, adhabu yake ni kifungo cha miaka saba (7) jela au faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar.

Hivi karibuni Wema amedaiwa kusambaza picha zenye maudhui ya kingono kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na mwanaume aliyedai kuwa ni ‘Future husband’ wake alifahamika kwa jina la Patrick Christopher ‘PCK’.

Aidha, siku chache zilizopita baada ya video hizo kuwa gumzo Wema alizungumza na vyombo vya habari na kuomba msamaha Watazania wote pamoja na Serikali yake na kudai kuwa anaomba radhi na kukiri hatorudia tena akiamini kuwa ulikuwa ni utoto na ujinga hivyo ameacha ujinga na utoto sasa amekuwa mpya.

Baraza la Sanaa Tanzania liliamua kumchukulia hatua stahiki kwa kumfungia kufanya kazi zake za filamu kwa muda usiojulikana.

 

Ndege nyingine aina ya Boeing 737 yaanguka Indonesia
Mwili wa Isaac Gamba unaagwa Lugalo muda huu