Northern Ireland inatajwa kuwa ni sehemu inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu kujiua idadi hiyo ni kubwa mara mbili ya ile ya Uingereza.
Idadi ya watu wanaojiua katika mji huo ni kubwa kulinganisha na idadi ya watu waliokufa kwa matukio ya kikatili yaliyoisha mwaka 1998 mara baada ya makubaliano ya amani kufanyika.
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Patricia Ferrin amesema familia yake ilivurugika mara baada ya watoto wake watatu kufariki dunia kwa kujiua wenyewe.
Ambapo mtoto wake wa mwisho Nail alijiua mwaka 2011 wa Pili, Kieran alijiua mwaka 2014 na mtoto wake wa kwanza Stephen alijiua mwaka 2017 ambapo Stephen alijiua akiwa na tatizo la akili.
Patricia alijitahidi kwa juhudi zake kuhakikisha anaokoa maisha ya mtoto pekee aliyebakia naye kwa kujaribu kumpeleka hospitali lakini siku mbili baada ya kumpeleka hospitali alikuta Stephen tayari amechukua maisha yake akiwa chumbani.
Ni vigumu kutambua sababu gani zinafanya mtu kuchukua maisha yake kwani kila aliyejiua hujiua kwa sababu zake na sababu hizi mara nyingi huwa za mtu binafsi.
Profesa wa chuo kikuu cha Ulster, Sioghan amefanya utafiti kugundua sababu inayopekea idadi kubwa ya watu wa Northen Ireland kujiua na kutaja moja ya sababu kuwa ni ugonjwa wa akili unaowakabili watu wengi katika eneo hilo la Marekani lakini ametaja sababu nyingine kuwa ni msongo wa mawazo.
Aidha dalili mbalimbali zimetajwa na watalaamu wanaoweza kutambua mtu anayekaribia kujiua ikiwa ni pamoja na kuongea peke yake, kucheka katika kila jambo liwe zuri au baya na kutokujali kuhusu yeye, wapweke, wasiopenda kuzungumza juu ya matatizo yao, mtu mwenye tabia hizo ni mtu ambaye amekata tamaa na muda wowote anaweza kuchukua uamuzi wa kukatisha maisha yake.
Hayo yamesemwa na moja ya wazazi waliopoteza watoto wao kwa kujiua wenyewe na kuamua kutoa mafundisho juu ya dalili za kuwatambua watu wa namna hiyo.