Nesi mmoja nchini Ujerumani amekiri mbele ya mahakama kwamba aliwaua wagonjwa takriban 100, hali inayomfanya kuwa miongoni mwa wauaji wakubwa kabisa kuwahi kutokea.
Wapelelzi wamesema kuwa, Neils Högel alikuwa akiwapatia wagonjwa wake dozi kali ambazo zilipelekea umauti wao katika hospitali mbili ambazo alikuwa akifanya kazi.
Aidha, lengo la nesi huyo, kwa mujibu wa wapelelezi ilikuwa ni kuwashangaza na kuwavutia wafanyakazi wenzie kwa kuwarejeshe fahamu wagonjwa aliowalaza kwa kutumia dozi kali, ambapo mchanganyiko huo wa dozi za kuwalaza na kuwaamsha ndio uliowaathiri zaidi wagonjwa.
Högel tayari anatumikia kifungo cha maisha kwa kosa la kusababisha vifo sita vya wagonjwa aliokuwa akiwahudumia.
Sasa inaaminika kuwa amewaua wagonjwa 36 katika mji wa Oldenburg na wengine 64 katika mji jirani wa Delmenhorst kati ya mwaka 1999 na 2005.
Hata hivyo, alipoulizwa na Jaji katika mahakama ya Oldenburg kama mashtaka yanayomkabili yana ukweli wowote, nesi huyo alikubali kutenda mashtaka yote hayo.
-
Ndege nyingine aina ya Boeing 737 yaanguka Indonesia
-
Angela Merkel atangaza kuachia ngazi 2021
-
Marekani yapeleka Wanajeshi 5,200 mipakani kuzuia wahamiaji