Mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain wanajipanga kuwasilisha ofa ya kumsajili kiungo Paul Pogba, kwa kuamini huenda ikawa ngumu kwa mchezaji huyo kurejea nchini Italia kwa ajili ya kujiunga tena na bingwa wa nchini humo Juventus.
PSG wanaamini watakua na nafasi kubwa zaidi ya kukamilisha mpango wa kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, kwa kutumia mazingira ya nchi yake ya Ufaransa, tofauti na Italia ambapo mara kadhaa aliripotiwa kufanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi.
Rais wa mmiliki wa klabu ya PSG Nasser Al-Khelaifi, anatajwa kuongoza mkakati wa kuhakikisha kiungo huyo anasajiliwa klabuni hapo mwezi Januari mwaka 2019, na tayari amejipanga kukutana na wakala wa Pogba, Mino Raiola.
Mara kadhaa kiongozi huyo amewahi kukaririwa akisema suala la usajili wa Pogba, ambaye siku za karibuni alikua hana raha kwenye kikosi cha Man Utd, kufuatia mikwaruzano iliyojitokeza kati yake na meneja Jose Mourinho.