Wanafunzi wawili wa shule ya sekondari Nsemlwa, iliyopo Manispaa ya Mpanda wamenusurika kujiua baada ya kulazimishwa na wazazi wao kuendelea na masomo.
Wanafunzi hao mmoja ni wakike aliyekuwa akisoma kidato cha kwanza na mwingine wa kiume aliyekuwa akisoma kidato cha pili, wanadaiwa kuwa watoro sugu na wametishia kujiua kwa kujinyonga au kunywa sumu iwapo wazazi wao na walimu wataendelea kuwalazimisha kwenda shule.
Mwanafunzi wakike alikutwa tayari amesha tundika kamba kwenye dali na kupanda kwenye kiti kwa ajili ya kujinyonga, walipo ulizwa sababu za kukataa shule hawakuwa nazo lakini waliendelea kushilikia msimamo wao wa kukataa kwenda shule,
kwa mujibu wa katibu wa Baraza la kata ya uwanja wa Ndege wa Manisipaa hiyo, Salum Msimani amesema kuwa wanafunzi hao tayari wamesha fikishwa kwenye Baraza la kata na kufunguliwa mashtaka ya utoro shuleni, lakini bado waliendelea na msimamo wa kutaka kujiua.
-
Video: Magufuli aanika utajiri Tanzania, Mbowe azidiwa
-
Mpanda kuanzisha bucha la kuuza nyama ya viboko
-
Treni yapata ajali jijini Dar
Hata hivyo, ameongeza kuwa Baraza hilo limeshindwa kutoa hukumu dhidi ya Wanafunzi hao wawili ambapo hata shuleni walipokuwa wanasoma walimu wao wamewainulia mikono pia Polisi wamefikishwa na wazazi wao lakini imeshindikana wameng’ang’ania msimamo wao.