Chama kikuu cha upinzani nchini Nigeria, Peoples Democratic Party (PDP) kimemkondi Brian Ballard mbaye ni mtaalamu wa mikakati aliyehusika katika kusaidia kampeni zilizompa ushindi Rais Donald Trump wa Marekani mwaka 2016 ili kuwawezesha kushinda uchaguzi wa urais mwakani.
Mtaalam huyo wa mikakati ya chaguzi za kisiasa anatarajiwa kumsaidia mgombea wa chama hicho, Atiku Abubakar kufanikiwa kuwa Rais wa Nigeria kupitia uchaguzi wa mwaka 2019.
Ballard, anayefahamika kwa mikakati yake ya hali ya juu anatajwa kuwa moja kati ya sababu zilizofanikisha ushawishi kwa wananchi waliomchagua Donald Trump kuwa Rais licha ya kupitia changamoto ya kuandikwa vibaya na vyombo vingi vya habari.
Kampuni ya Ballard imesaini mkataba na PDP ambapo itakuwa ikilipwa $90,000 (sawa na N31.5m) kila mwezi. Mkataba huo ambao unatarajiwa kudumu kwa mwaka mmoja utaigharibu PDP zaidi ya $1 milioni.
-
Mourinho atamba baada ya kuipiga Bournemouth, ‘msiniongezee mvi’
Kwa mujibu wa BBC, Waziri wa zamani wa anga wa nchi hiyo ambaye hivi sasa ni mpinzani wa Serikali, Osita Chidoka ndiye aliyesaini mkataba huo kwa niaba ya PDP.
2019: PDP Hires Donald Trump’s Presidential Campaign Strategist, Brian Ballard https://t.co/o0Mwvy1Fwa
— Oriental Times (@OrientalTimes) November 2, 2018
Ikumbukwe kuwa mwaka 2014, chama tawala cha All Progressive party (APC) kiliikodi kampuni ya AKPD ya Marekani ambayo ilifanya kazi ya kusaidia kampeni za Barack Obama ikijihusisha na masuala ya vyombo vya habari pamoja na jumbe.